Maelfu ya abiria wakwama kusafiri JKIA Kenya

|
Baadhi ya wasafiri wanaotumia uwanja wa Jomo Kenyatta wakiwa wamekwama nje ya uwanja huo kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege

Maelfu  ya abiria wamejikuta wakiwa hawajui la kufanya katika viwanja vyote vinne nchini Kenya baada ya kutokea mgomo wa wafanyakazi uliosababisha usumbufu mkubwa wa ndege.

Wafanyakazi hao waliogoma leo wamesema, hawajafurahia kuhusu mpango wa kuziunganisha mamlaka za viwanja vya ndege na Shirika la Ndege la Taifa.

Takribani ndege 60 zimeshindwa kupaa leo, Jumatano kutoka kwenye Uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa  Jomo Kenyatta ambao ni uwanja mkubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kulazimika kutua katika Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam.  Huku kukidaiwa kuwepo kwa baadhi ya ndege kukosa abiria kabisa.

Viwanja vya ndege vya Mombasa, Eldoret na Kisumu nazo pia zimedaiwa kupatwa na usumbufu huo.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imelaani mgomo huo na kusema ni kinyuma na sheria.  Aidha imesema, utaratibu unafanyika wa kuwapeleka watumishi wengine kuweka sawa hali iliyopo.

Inasemekana kuwa, polisi wamepelekwa katika uwanja wa ndege wa Nairobi na kuwarushia mabomu ya machozi wafanyakazi hao waliokuwa katika mgomo.

Kiongozi mkuu aliyeratibu  mgomo huo kutoka Chama cha Umoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Anga nchini Kenya ambaye ni Katibu mkuu, Moss Ndiema, amekamatwa.

Biashara
Maoni