Mahakama Kuu Kigali yawaachia huru Diana Rwigara na mama yake

|
Washtakiwa Diana Rwigara (wa pili kushoto waliokaa) akiwa na mama yake, aliyesimama wakifurahia jambo baada ya kupatiwa dhamana

Mahakama Kuu mjini Kigali imewaachilia huru mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mama yake waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na kughushi nyaraka.

Jaji wa Mahakama Kuu mjini Kigali ametangaza uamuzi huo baada ya kukutwa hawana hatia.

 

Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na kuligawa taifa miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka za serikali wakati wa kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Urais mwaka jana.

Wawili hao wakati wote wamekuwa wakikanusha kuhusu mashtaka hayo na kudai kuwa kesi yao hiyo inachochewa na sababu za kisiasa.

Mahakamani
Maoni