Mahakama yatengua uamuzi wa kufungiwa maisha Michael Wambura

|
Michael Richard Wambura ambaye aliamua kwenda katika mahakama za kiraia kupinga kufungiwa kwake.

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetengua uamuzi ya Kamati ya Maadili za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumfungia maisha kujihusisha na mchezo huo, aliyekuwa Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura.

Uamuzi huo umetolewa leo katika mahakama hiyo na Jaji Benhajji Masoud kufuatia kesi iliyofunguliwa na Wambura kupinga kufungiwa maisha na Kamati za Maadili za TFF.

Kwa uamuzi huo, Wambura anarejea katika madaraka yake ya Umakamu wa Rais wa TFF na Uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara FAM.

Machi mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wake wa wakati huo, Hamidu Mbwezeleni ilimfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka kwa kumtuhumu kwa makosa matatu.

Makosa hayo ni kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF.

Soka Tanzania
Maoni