Majeshi ya Tanzania Darfur yamwagiwa sifa

|
Askari wa JWTZ waliopo kwenye vikosi vya Umoja wa Mataifa wakiwa kazini.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Amani katika Jimboni Darfur, Luteni Jenerali Leonard Ngondi amesifu kazi nzuri inayofanywa na askari wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID) kutoka Tanzania  ambao amesema ni kielelezo cha mafaniko ya Operesheni ya Darfur.

Luteni Jenerali Ngondi ametoa pongezi hizo wakati akihitimisha ziara yake katika Kikosi cha Tanzania katika kambi iliyoko Menawashe.

Aidha amesema kufuatia zoezi la kupunguza vikosi katika Ulinzi wa Amani, kwenye Jimbo la Darfur  kazi za ulinzi wa amani kwa sasa zitahamia katika eneo la Jaber Mara Mashariki ambapo kimeundwa kikosi kazi kitakachohusisha kambi kumi zinazozunguka eneo hilo ikiwemo kambi zinazokaliwa na  Jeshi la Tanzania huku maeneo mengine yakifungwa.

Amezitaja kambi hizo kuwa ni pamoja na Minawashi, Khor, Abeche na Shangilitobaya zinazokaliwa na wanajeshi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo lilipongezwa kwa kufika maeneo hayo kwa ajili ya kuangalia miundombinu na kutathmini.

Mkuu huyo wa majeshi ya ulinzi amezitaja kambi nyingine kuwa ni Kass,Tawila,Kapya,Sontoni, Golo ,Netiti na Jalinje ambayo itakuwa Makao Makuu ya Task Focre hiyo yenye lengo la kuhahakisha huduma ya UNAMID inawafikia wakazi wa Jaber Mara ambao maeneo yao hayakufikika kutokana na miundombinu iliyowafanya waasi kujiimarisha katika mapigano.

Utawala
Maoni