Man United uso kwa uso na Barcelona robo fainali Ulaya

|
Manchester United imeshinda mchezo mmoja pekee katika michezo minane ambayo imekutana na Barcelona.

Droo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepangwa mchana wa leo, Mjini Nyon Uswisi ikishuhudiwa miamba minane barani humo ikifahamu inakwenda kukutana na kibarua gani.

Katika droo hiyo, vigogo wawili wa Soka barani humo, Manchester United na FC Barcelona wamepangwa kukutana ambapo Man United wataanzia nyumbani. 

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Manchester United imeshinda mchezo mmoja pekee katika michezo minane ambayo imekutana na Barcelona, ikifungwa mitatu na kutoka sare minne.

Matokeo kamili ya droo hiyo ni kama ifuatavyo:-

Man United vs Barcelona.

Liverpool vs FC Porto.

Tottenham vs Man City

Ajax vs Juventus.

Kwenye hatua ya nusu fainali atakayeshinda kwenye mchezo kati ya Barcelona na Man United atakutana na mshindi kati ya Liverpool na FC Porto  wakati mshindi wa mchezo kati ya Tottenham na Man City atakutana na mshindi katika mchezo wa Ajax na Juventus.

Katika hatua nyingine droo ya robo fainali katika michuano ya Europa League pia imefanyika ambapo Arsenal na Chelsea wamewajua wapinzani wao huku timu mbili za Hispania zikikutanishwa.

Matokeo ya droo hiyo ni kama ifuatavyo:-

Arsenal vs Napoli.

Villarreal vs Valencia.

Benfica vs Frankfurt.

Slavia Praha vs Chelsea.

Kwa upande wa nusu fainali matokeo yako namna hii:-

Arsenal/Napoli vs Villarreal/Valencia.

Benfica/Frankfurt vs Slavia Praha/Chelsea.

UEFA
Maoni