Mapacha wazaliwa wakiwa wameungana Geita

|
Watoto wa kike waliozaliwa jana, Machi 18, 2019 wakiwa wameungana

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Theodora Wilson ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Kasuguya, Kata ya Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita amejifungua watoto watatu wa kike kati yao wawili wakiwa wameungana.

Akizungumzia tukio hilo, mama wa watoto huyo amesema kwa muda mrefu alikuwa akimuomba Mungu aweze kumjalia kuzaa mapacha na anayofuraha kuu hatimaye kilio chake kimejibiwa.

Mama huyo ambaye alitokea katika Hospitali ya Kharumwa wilayani Nyang’hwale baada ya kushindwa kujifungua, alifikishwa katika Hospitali hiyo Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kufanikiwa kujifungua mtoto wa kwanza kwa njia ya kawaida kabla ya kubainika kuwepo kwa watoto wa ziada ambao alijifungua kwa njia ya upasuaji.

Watoto hao watatu wamezaliwa jana, Machi 18 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Hospitali Teule ya Rufaa Mkoa wa Geit

Daktari Joseph Makuma wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa Wa Geita, amethibitisha kuzaliwa kwa watoto hao na kuongeza kuwa wana afya njema na kwamba licha ya kuungana katika maeneo ya kifua kila mmoja anajitegemea katika matumizi ya viungo vyake vyote

Dk. huyo amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Geita na kwake pia.

Imeelezwa kuwa  watoto hao ni uzao wa pili kwa mwanamke huyo na katika kipindi cha ujauzito wake alipata shida za kuelemewa na tumbo hali iliyomfanya kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi zaidi ambapo madaktari walibaini uwepo wa mapacha.

Maisha
Maoni