Marekebisho sheria ya vyama vya siasa 'mtihani' kwa watakaoungana

|
Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza (kushoto). Picha na Maktaba

Vyama vya Siasa Nchini huenda vikalazimika kufa iwapo viongozi wake na wanachama wao watahitaji kutengeneza muungano kuelekea kwenye chaguzi na hivyo kutakiwa kuunda Chama kipya ambacho kitapata usajili kulingana na mkataba wa makubaliano watakaofikia.

Haya ni sehemu ya matakwa ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2018 kupitia muswada wake uliowasilishwa Bungeni mwezi Novemba mwaka huu ambapo sasa hakutakuwa na uhuru wa vyama kuungana kiholela badala yake kwa kufuata masharti ya kisheria.

Hayo yamebainika leo, Alhamisi katika mahojiano maalumu kati ya Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza na Azam TV waliotaka kufahamu faida na adhari zinazoweza kujitokeza kufuatia sheria hiyo.

Akitolea ufafanuzi suala hilo lililotokana na hofu ya kuwa sheria hiyo inaweza kuua upinzani na kurudisha mfumo wa Chama kimoja, Msajili msaidizi huyo amesema marekebisho yaliyofanyika yana nia njema ya kuviimarisha vyama vya upinzani na kukanusha madai ya kwamba yanalenga kuua mfumo wa vyama vingi nchini kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

Siasa
Maoni