Matumizi holela ya dawa yatajwa kuchangia maradhi ya figo nchini

|
Utumiaji holela wa dawa sababu ya matatizo ya figo

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya afya ya figo duniani ugonjwa huo unaelezwa kushika nafasi ya sita katika magonjwa yanayosababisha vifo kutoka nafasi ya 18 ya awali huku sababu kubwa ya kuongezeka kwa ugonjwa huo ikitajwa ni matumizi mabaya ya dawa za kutuliza  maumivu na vileo.

Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile alipohudhuria maadhimisho ya siku hii ambapo amesema  Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kutumia dawa kiholela bila ya kupima na kufuata ushauri wa daktari .

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini kwa maeneo ya kaskazini, asilimia saba ya Watanzania wana ugonjwa wa figo huku kidunia asilimia 13 ya watu wana ugonjwa huo.

Kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo, naibu waziri huyo amesema kwa sasa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inafanya upandikizaji wa figo na tayari imeshafanikisha kuwawekea wagonjwa 38 tangu ilipoanza kutoa huduma hiyo.

Afya
Maoni