Mbeya yakabiliwa na uhaba wa madawati 7000

|
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya jiji la Mbeya, Vicent Msola akipokea madawati 40 kutoka kwa mchoraji maarufu, Ali Richard kutoka mradi wa Niache Nichore

Halmashauri ya Jiji la Mbeya ina upungufu wa madawati zaidi ya 7000 kwa shule za sekondari ambao umetokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaofaulu kuingia kidato cha kwanza kufuatia serikali kutoa elimu bure.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya jiji la Mbeya, Vicent Msola ametoa kauli hiyo wakati akipokea madawati 40 kutoka kwa Msanifu wa Michoro, Ali Richard kupitia mradi wake wa Niache Nichore.

Jiji la Mbeya ni miongoni mwa mikoa iliyokumbana na ongezeko la wanafunzi kwa kiwango kikubwa huku wengi wa wanafunzi hao waliomaliza shule ya msingi wakikabiliwa na ukosefu wa madarasa na madawati ya kusomea.

Elimu
Maoni