Mgogoro wa eneo la makaburi kupatiwa ufumbuzi

|
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed akijibu swali kuhusu mwekazaji kuvunja ukuta wa makaburi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema tayari imeanza kulichukulia hatua hatua mbali mbali tatizo la mgogoro wa eneo la makaburi kwa wananchi wa matemwe na mwekezaji aliyevamia eneo hilo.

Akijibu swali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani,Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema miongoni mwa hatuà hizo ni pamoja na kuundwa Kamati ya Mawaziri kwaajili ya kufanya mazungumzo na mwekezaji aliyedaiwa kuvunja ukuta uliokuwa umezunguka makaburi ili kurejesha ukuta huo na kukubali kuujenga upya

Dkt. khalid amesema kuwa Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) hairuhusu uwekezaji ambao unakwenda kinyume na matakwa ya wananchi hususan katika wakati wa sasa unaozingatia kuwa maeneo ya makaburi ,mizimu,  na mapango huhitaji kutunzwa kama sehemu ya mila na utamaduni wa nchi.

Dkt. Khalid Salum Mohammed amewataka wananchi kuheshimu maeneo ya utamaduni yakiwemo makaburi na kuwaonya wale wanavunja sheria kwa makusudi kwa kubadili matumizi ya maeneo hayo kuwa serikali haitawafumbia macho.

Aidha ushauri umetolewa kuwa maeneo hayo ya makaburi yazungushiwe ukuta ili kutoruhusu uvunjifu wa sheria na kuwataka wawekezaji kufuata masharti wanayopewa kwa lengo la kuondoa uvunjifu wa amani.

Utawala
Maoni