Mgogoro wa madiwani na DC wadaiwa kuumiza wananchi

|
Miongoni mwa athari za kususiana zilizoukumba mji wa Tunduma, mirundikano ya taka, wananchi kutokua la kufanya.

Mgogoro kati ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma na Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Irando umetajwa kuchangia kusimama kwa shughuli za maendeleo katika mji wa Tunduma ikiwemo uzoaji taka ambazo zimeachwa kwa muda mrefu huku zikitoa harufu kali kutokana na kukosa usimamizi.

Takribani miezi saba imeshapitia sasa tangu halmashauri hiyo itoe tamko la kutompa ushirikiano mkuu  huyo wa wilaya.

Kwa muda huo wote kumekuwa na mvutano wa pande zote mbili, huku baraza la mji likishindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi na hivyo wananchi wengi kukosa haki na huduma za msingi zikiwemo pamoja na za kujiletea maendeleo.

Miongoni mwa viongozi hao wamesema, wameona waumalize mgogoro huo kutoka na kuona wazi kuwa umekuwa na athari na kwamba kazi zao zinategemeana ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo baada ya kutunishiana misuli hatimaye uongozi wa halmashauri hiyo umekubali yaishe, na sasa wametangaza rasmi kuondoa zuio lao na kukubali kushirikiana na mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wa wananchi walioongea na AZAM TV wamewataka viongozi hao kufanyakazi kwa ushirikiano kwa sababu waliwachagua kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na kuacha kuingiza masuala ya siasa katika mustakabali wa maendeleo ya wananchi.

Utawala
Maoni