Mkurugenzi mtendaji awatoa hofu wateja wa Boeing 737

|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Boeing, Dennis Muilenburg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Boeing, Dennis Muilenburg amewahakikishia usalama wateja na abiria wake licha ya ndege zake mbili kwa nyakati tofauti kupata ajali nchini Indonesia na Ethiopia.

Ameyasema hayo kupitia ujumbe wa video uliochapishwa katika kipindi cha uchunguzi mkali kufuatia ajali ya ndege ya Ethiopia airline.

Ajali hiyo iliyohusisha Ndege ya Ethiopia ya Boeing 737 MAX 8 iliua watu 157 chini ya miezi sita baada ya ndege ya aina hiyo ya Kampuni ya Lion Air kuanguka na kuua watu 189.

Kutokea kwa ajali hizo mbili umeiweka lawamani Kampuni ya Boeing kwamba huenda ilichelewa kurekebisha tatizo la kimfumo lililobainika baada ya ajali ya Lion Air.

“Wakati inapotokea ajali kwa sababu yoyote, sisi huzingatia bila kusita kubaini sababu ya ajali husika. Tunaungana na wateja wetu, wasimamizi wa kimataifa na mamlaka za serikali katika jitihada zetu za kusaidia uchunguzi wa hivi karibuni, kuelewa ukweli wa kile kilichotokea na kusaidia kuzuia madhara ya baadaye. " alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Boeing, Dennis Muilenburg. 

Usafiri
Maoni