Mkutano Mkuu TFF wasogezwa mbele

|
Mkutano huo utafanyika palepale mjini Arusha kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Kamati ya Utenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesogeza mbele Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo uliokuwa umepangwa kufanyika Desemba 30, 2018 mjini Arusha na sasa utafanyika Februari 2, 2019.

Taarifa iliyotolewa leo na TFF imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kuendana na kalenda ya uchaguzi mdogo uliotangazwa na kamati hiyo.

Uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Lindi na Mtwara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Simiyu na Shinyanga.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu limeanza Disemba 4, 2018 mwisho ikiwa Disemba 9, 2018.

Soka Tanzania
Maoni