Moto wa Samatta haukamatiki Ubelgiji

|
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta alipokuwa akiifungia timu yake moja kati ya mabao katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Besiktas

Mbwana Ally Samatta jana ameifungia KRC Genk magoli mawili na kutengeneza moja dhidi Besiktas.

Kwa sasa Mbwana Samatta amecheza mechi 8 za Uefa Europa League na kufunga magoli 9 na kutoa assists 2.

Hatua ya kufuzu alifunga magoli 6 na Assist 1 na makundi magoli kafunga 3 na Assist 1.

Kwa msimu huu Samatta amehusika katika magoli 18 (16 goals, 2 Assists) katika mechi 18.

Hadi sasa Samatta amefikisha magoli 50+ ndani KRC Genk katika mechi 130 na anakuwa mfungaji bora namba 6 wa muda wote wa Genk.

Soka
Maoni