Mrema awapa mtihani Polisi na TCRA

|
Mwenyekiti wa Parole, Augostino Mrema akitoka katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, AUGUSTINO MREMA ameziomba mamlaka husika kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuzusha habari za uongo ambazo zinachafua majina ya watu.

Mrema amesema hayo jijini Dar es salaam leo, Ijumaa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ambapo alifika kwa ajili ya kutoa  taarifa  dhidi ya watu waliomzushia kifo.

Aidha amesema kuwa ni vyema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuweka adhabu kubwa kwa watu wanaopatikana na makosa ya matumizi mabaya ya mitandaoni  ili iwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya kufanya hivyo.

Uhalifu
Maoni