Msalaba mwekundu yahofia baa la njaa Korea Kaskazini

|
Hali ya ukame iliyoikumba nchi ya Korea Kaskazini

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba mwekundi limetangaza janga kwa nchi ya Korea Kaskazini, kufuatia mazao yaliyopandwa kama mpunga, mahindi na mengineyo kuathiriwa na hali ya joto kali.

Ikitangazwa hali hiyo leo, Ijumaa, shirikisho hilo limeonesha mashaka yake hayo kwa kusema, kunauwezekano wa kutokea kwa janga kubwa na kuonya hatari ya kutokea kwa uhitaji mkubwa wa usalama wa chakula kwa nchi hiyo ambayo imetengwa kufuatia kuwekewa vikwazo na jumuiya za kimataifa.

Nchi hiyo imekosa mvua tangu Julai huku hali ya joto ikiendelea kupanda na kufikia kiwango cha kipimajoto 39 katika nchi nzima, hata hivyo taarifa kutoka serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea kaskazini imesema walitegemea mvua katikati ya mwezi Agosti.

Idadi kubwa ya watu milioni 25 tayari wanadaiwa kuwa katika mashaka na hatari ya watoto kupatwa na utapiamlo hali inayoweza kuwa mbaya zaidi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya shirikisho hilo lililo na makao makuu yake huko Geneva.

 “Hatuwezi kuiacha hali hii ikisababisha ukosefu wa chakula kabisa. Tunafahamu athari za awali zilivyokuwa mbaya na kufikia mahali ikisababisha tatizo kubwa la afya na utapiamlo kwa nchi nzima,” alisema kiongozi wa shirikisho hilo kupitia taarifa hiyo.

Tayari shirikisho hilo limeshaanza kuisaidia shirika la kitaifa la msalaba mwekundu nchini humo kupeleka misaada katika sehemu zilizohatarini zaidi na kupeleka timu ya dharura ya kutafuta suluhu pamoja na mashine za kunyonya maji 20 zitakazosaidia kumwagilia maeneo ambayo yamekumbwa zaidi na ukame uliotokana na joto hilo.

David Beasley, Kiongozi wa Umoja wa Mataifa anayesimamia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), alitembelea nchi hiyo mwezi Mei na kuangalia namna ambavyo wataweza kusaidia kusambaza chakula kwa wanawake na watoton, katika dalili hizi za awali.

Korea Kaskazini ilishawahi kupatwa na janga la njaa katikati ya mwaka 1999 na kusababisha vifo vya watu takribani milioni tatu.

Chakula
Maoni