Mshukiwa wa shambulio lililoua 49 New Zealand afikishwa mahakamani

|
Mshukiwa wa shambulio la misikiti miwili nchini New Zealand raia wa Australia, Brenton Tarrant mwenye miaka (28) akiwa mahakamani

Mshukiwa mkuu wa shambulio lililoua watu 49 katika mashambulizi ya risasi katika misikiti miwilinchini New Zealand jana, Ijumaa amefikishwa mahakamani akikabili na shtaka la mauaji.

Mshukiwa huyo raia huyu wa Australia, Brenton Tarrant mwenye miaka (28), alifikishwa mahakamani hapo akiwa katika mavazi meupe ya kifungwa huku akiwa na pingu mikononi.

Mashtaka zaidi yanatarajiwa kufunguliwa dhidi yake.

Waziri mkuu, Jacinda Ardern amesema Tarrant alikuwa na bunduki tano kwa ajili ya kutekeleza unyama huo na milipuko ambavyo vyote vilikuwa na leseni ya umiliki, na kuongeza kuwa : " Sheria zetu za umiliki wa silaha zitabadilishwa."

Wengine wawili wako chini ya ulinzi, huku kati yao hakuna aliye na rekodi ya uhalifu.

Tarrant, ameelezewa kama mzungu mwenye itikadi kali na alisimama kimya wakati wote wa kutolewa maelezo mafupi mahakamani.  Mara baada ya kesi hiyo, mshukiwa huyo amerudishwa rumande na anatarajiwa kurudishwa tena mahakamani Aprili 5.

Waziri mkuu wa nchi hiyo ameliita shambulio hilo la Christchurch "tukio la kigaidi". Mamlaka nazo bado zinaendelea na zoezi la kuwatambua waathirika wa shambulio hilo.

Mahakamani
Maoni