Msimu mpya ligi ya wanawake kuanza Desemba 29

|
Mabingwa wa msimu uliopita kwenye Ligi ya Wanawake, JKT Queens.

Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa upande wa wanawake inatarajia kuanza kutimua vumbi Desemba 29 mwaka huu ikishirikisha timu 12 badala ya nane (8) zilizoshiriki msimu uliopita.

Huu ni msimu wa tatu wa ligi hiyo ambapo msimu wa kwanza na wa pili ilichezwa kwa mtindo wa makundi huku msimu huu ikitarajiwa kuchezwa kwa mtindo wa mzunguko.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa soka la wanawake Amina Karuma amesema ligi ya msimu huu itakuwa na msisimko zaidi kutokana na maandalizi ya timu shiriki.

Kwa upande wa Mkurungenzi wa Ufundi wa TFF Ammy Ninje amesema ligi hiyo ni mwanzo mzuri wa kutengeneza timu imara ya taifa.

Msimu wa kwanza wa ligi hiyo ulishuhudia Mlandizi Queens wakiibuka mabingwa huku JKT Queens wanaingia katika msimu huu wa tatu wakiwa mabingwa watetezi baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.

Soka la wanawake
Maoni