Msimu wa pili SZIFF wazinduliwa, Jokate awa Mlezi

|
Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Serena, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (Kulia) amechaguliwa kuwa mlazi wa tuzo hizo.

PRESS RELEASE;

Maandalizi ya msimu wa pili wa tamasha la tuzo za kimataifa za Sinema Zetu yamekamilika.

Tamasha hili limepangwa kuanza tarehe 1/1/2019 mpaka tarehe 15/1 /2019 na kuhitimishwa na “usiku wa tuzo” ambao utafanyika tarehe 23/2/2019 katika ukumbi wa Mlimani City. Tamasha hilo litaonyeshwa mubashara na Azam TV kupitia chaneli ya  Sinema Zetu.

Akizungumzia tamasha hili, Afisa Mtendaji Mkuu wa Uhai Productions Bw. Tido Mhando alisema kuwa kipekee amejivunia namna msimu wa kwanza wa tamasha hili ulivyoamsha ari na hamasa kwa waandaaji na wapenzi wa filamu.

Hili ni tamasha la kwanza la filamu Afrika kuonyeshwa kwenye televisheni, filamu zitashindanishwa kwenye vipengele tofauti tofauti huku ushindani ukiaminika kuwa mkubwa Zaidi ya msimu uliopita kwakuwa moja ya vigezo vya filamu zitakazoshindanishwa ni kuwa lazima ziwe zimeandaliwa kati ya mwaka 2016 na 2018. Hii itatupa picha halisi ya ufanisi na bora wa uandaaji wa filamu, amesema Tido Mhando.

Mkurugenzi wa Tamasha Bw. Jacob Joseph amesema kuwa Kiswahili ni miongoni mwa Lugha kumi kubwa  kuzungumzwa Barani Afrika. Matamasha mengi hayajakidhi kuwafikia watu wengi na kuwatimizia mahitaji yao kupitia Sanaa.

Aidha Bw. Jacob ameongeza kuwa tamthilia za Kiswahili kwenye televisheni zimejizolea umaarufu mkubwa kwa watazamaji. Hivyo ili Kupima ufanisi wake mwaka huu, kimeongezeka kipengele kipya cha Tamthilia kwenye Tamasha kijulikanacho kama, Tuzo za Tamthilia za kimataifa za Azam TV. Tuzo hizi zitatolewa kwa Tamthilia Bora, Moungozaji Bora, Muandishi Bora, Muigizaji Bora wa kike na wa kiume.

Akielezea malengo ya tamasha, MratibU wa Tamasha, Bi. Sophia Mgaza amesisitiza kwamba dhumuni kuu ni kuleta soko la filamu na televisheni pamoja chini ya mwamvuli mmoja, “lugha moja, tamasha moja”. Tumewaataarifu waandaaji kuwasilisha kazi zao za kibunifu kwa ajili ya tamasha hilo. Aidha uwasilishaji  utafunguliwa rasmi tarehe 1 Octoba mpaka 30 Novemba, 2018. Mchakato wote una baraka za COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania.

Mwenyekiti wa jopo la majaji ni Profesa Martin Mhando, yeye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa jopo la majaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar.

Mchakato wa kutoa tuzo utasimamiwa na jopo la majaji ambao watachambua na kuainisha washindi kulingana na vigezo vilivyowekwa.

Filamu
Maoni