Mtoto azawaliwa akiwa na mguu mmoja Rombo

|
Kichanga kilichozaliwa kikiwa na mguu mmoja kikipatiwa huduma katika Hospitali ya Huruma wilayani Rombo, Kilimanjaro

Mwanamke mmoja mkazi wa Ibukoni wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro amejifungua mtoto mwenye mguu mmoja wa kulia lakini mwenye afya njema ambaye ni uzao wake wa kwanza.

Devota Swai mwenye umri wa miaka 25 amejifungua mtoto huyo wa kike Desemba 28 mwaka jana katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma wilayani humo.

Mama huyo ameoneshwa kushtushwa na hali hiyo na kuiomba jamii na serikali kumsaidia kukabiliana na tatizo hilo la mwanaye hususan vifaa kama mguu wa bandia, kigari pamoja na fedha za kumsaidia kujikimu na mtoto huyo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi katika hospitali hiyo ya Dk. Wilbold Kyejo akieleza sababu za kisayansi za matokeo ya uumbaji huo amesema, mara nyingi matatizo hayo hutokana na sababu za kibailojia katika muunganiko wa seli maarufu kama (choromosome) zinazotakiwa kutoka kila upande kwa baba na mama na inapokosekana upande mmoja ndipo hitilafu kama hizo za kukosa baadhi ya viungo hutokea.

Maisha
Maoni