Museveni aamuru wanaoishi maeneo hatarishi kuhamishwa

|
Rais Yoweri Museveni akisalimiana na kuwajulia hali wananchi wa Bududa walikumbwa na maafa ya mafuriko nchini Uganda

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni  ameamuru watu wote wanaoishi maeneo hatarishi kwenye milima ya Bududa kuhamishwa mara moja.

Agizo hilo linafuatia maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40 mpaka sasa.

Zaidi ya watu 1000 wameathirika kutokana na maporomoko hayo yaliyoikumba nchi ya Uganda Alhamisi iliyopita.

Mara ya mwisho tukio kama hilo lilitokea mwaka 2010 ambapo zaidi ya watu 100 walifariki dunia.

Mafuriko
Maoni