Mvua kubwa yaleya majanga mkoani Mbeya

|
Wakazi wa maeneo ya Nzovwe wakiwa katika harakati za kutoa maji ya mvua yaliyoingia ndani ya nyumba zao

Baadhi ya wakazi wa Kata za Nzovwe na Simike mkoani Mbeya hawana makazi baada ya nyumba zao kubomoka kutokana na mvua iliyonyesha jana kwa takribani dakika 20 tu.

Mvua hiyo iliyonyesha katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mbeya iliambatana na upepo mkali huku maeneo mengine ikinyesha mvua ya mawe.

Wakazi walioathiriwa na mvua hizo wamesema kwa sasa baadhi yao hawana chakula baada ya akiba waliyokuwa nayo kusombwa na maji na kuiomba Serikali iangalie uwezekanao wa kuwasaidia.

Wakazi hao wamesema, hali hiyo imetokea katika siku za hivi karibuni kutokana na ujenzi holela na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Mafuriko
Maoni