Naibu waziri Mabula awakumbuka walemavu wa ngozi Karagwe

|
Naibu waziri wa ardhi, Angelina Mabula akiwakabidhi watoto wenye ulemavu wa ngozi vifaa vya kujikinga na jua

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amewakabidhi vifaa vya kulinda ngozi watu wenye ulemavu wa ngozi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Mabula alitoa vifaa hivyo jana baada ya kuombwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi katika wilaya za Mkoa wa Kagera.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo kwa watu  hao wenye ulemavu wa ngozi, Naibu waziri Mabula aliipongeza Wilaya ya Karagwe kwa kuona uhitaji wa kundi hilo maalumu kwa kuwapatia vifaa vya kujilinda.

Alisema, watu wenye ulemavu wa ngozi wana changamoto nyingi lakini wilaya hiyo imeona umuhimu wa kuwapatia walemavu hao vifaa vya kujikinga na jua kuwa ni jambo jema na linaloweza kuwapa faraja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Godfrey Mheluka alisema pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi kutembelea wilaya yake kwa ajili ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi ameona atumie fursa hiyo kuwapatia walemavu hao wa ngozi vifaa lengo likiwa ni kuonesha kuwajali watu hao.

Maisha
Maoni