Nchi 13 kusheherekea kiaina wiki ya 'Fancophonie' jijini Dar es Salaam

|
Mabalozi wa nchi zinazozungumza Kifaransa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Juma la Francophonie
Katika kusheherekea wiki ya kuzungumza lugha ya Kifaransa nchini Tanzania shughuli mbalimbali zimeratibiwa zikihusisha jumla ya mataifa 13 yanayozungumza lugha hiyo.
 
Wakizungumza mapema wiki hii, mabalozi wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa nchini wamesema kwa nyakati tofauti kuwa wameona washeherekee lugha hiyo kwa kuandaa matukio mbalimbali yakiwemo ya michezo, maonesho ya filamu, chakula, dansi na makala zenye lengo la kuhamasisha lugha hiyo na utamaduni.
 
Miongoni mwa shughuli zitakazooneshwa jijini Dar es Salaam, ni pamoja na mashindano ya mpira wa soka kati ya timu za mabalozi wa nchi zinazozungumza Kifaransa yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, filamu zilizojizolea umaarufu za Cleaners, Intouchable, Hochelaga, Lands of Souls, Francophonie Encounters filamu zote zitazooneshwa bure sambamba na tamasha la muziki litakalohitimisha juma hilo, katika Ukumbi wa Nkurumah UDSM jijini Dar es Salaam.
 
Katika mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mabalozi hao wa nchi ya Ufaransa, Ubelgiji, Burundi,, Canada, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Misri, Morocco, Rwanda, Senegal, Shelisheli, Uswisi na Vietnam wamesema, lugha ya Kifaransa ni ya tano kati ya lugha inayozungumzwa sana duniani kwenye mataifa 32 na inakadiriwa ifikapo mwaka 2050 itakuwa ikizungumza na watu takribani milioni 700 kutoka idadi ya sasa ya watu milioni 300.
 
Tanzania ikiwa ni nchi iliyopakana na jirani zake wanaozungumza lugha hiyo maarufu kama 'Francophonie' imekuwa ni miongoni mwa nchi yenye nafasi kubwa ya kuwepo kwa fursa ya watanzania wengi kujifunza lugha hiyo katika vituo vilivyopo jijini Dar es Salaam na Arusha ambayo pia lengo lake ni kubadilisha tamaduni, elimu na kufurahia ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo na wananchi wake.
Tamasha
Maoni