Ndugai amwaga vifaa vya elimu jimboni kwake Kongwa

|
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa akikabidhi moja ya kompyuta alizozitoa katika shule zilizopo jimboni mwake

Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai leo, Machi 24 amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea Shule ya Sekondari Banyi Banyi iliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo, Ndugai alifanikiwa pia kutembelea shule nyingine zilizopo wilayani Kongwa na kugawa vitendea kazi mbalimbali vikiwemo vitabu, jezi, mipira, Kompyuta na Printa.

Mbunge huyo wa Kongwa pia alipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi wa shule hizo na kuwahimiza kusoma kwa bidi kwa amanufaa yao na taifa kwa ujumla

Elimu
Maoni