NEC yamteua Diwani Viti Maalum Temeke

|
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Athumani Kihamia alisema

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Fatuma Michael Shija kuwa Diwani wa Viti Maalum (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

“Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya aliyeteuliwa awali kufariki dunia,” Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Athumani Kihamia alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Shija aloiteuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa.

Siasa
Maoni