Neil Bush awataka Wamarekani kusheherekea maisha ya baba yake

|
Aliyekuwa Rais wa Marekani, George HW. Bush ambaye amefariki dunia Ijumaa

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Marekani, George HW. Bush, Neil Bush amewataka wamarekani kusherehekea maisha ya baba yake ambaye ameyaishi kwa miaka 94.

Neil Bush amesema hayo wakati mwili wa marehemu baba yake ukisafirishwa tayari kuelekea kwenye ibada maalum huku akimtaja kuwa alikua ni mtu wa watu.

Neil Bush, mtoto wa rais wa zamani wa Marekanif George H.W. Bush alinukuliwa akisema, "Baba yangu alikua mtu wa pekee, alipanga kila kitu na alifanya vyote kwa mapenzi ya hali ya juu, Alijali sana taifa lake, watu wake na ulimwengu kwa ujumla na alijitoa sana kuhudumia jamii, kuwanyanyua wengine ,hivyo vyote vina thamani sana na ndivyo nitavifuata na kuviendeleza.''

Rais huyo mstaafu alifariki huko Houston  Texas mwishoni mwa Juma na mwili wake umesafirishwa kutoka  Houston kuelekea  Maryland.

Ndugu na jama akiwemo mwanae  huyo wameondoka na mwili huo ambapo baadae ibada maalum itafanyika huko Washington .

Maisha
Maoni