Ocean Road waanza kutoa huduma za matibabu ya moyo

|
Daktari Bingwa wa mionzi, Tausi Maftaha akizungumzia upatikanaji wa huduma ya tiba ya moyo katika Hospitali ya Ocean Road

Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam imeanza kutoa huduma ya matibabu ya moyo ili kuimarisha huduma hizo nchini baada ya wagonjwa wengi kufuata huduma hiyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kutambulisha rasmi huduma hiyo mpya itakayosaidia wagonjwa wengi wanaopatiwa huduma ya matibabu katika hospitali hiyo ya Saratani jijini Dar es Salaam,Daktari Bingwa wa mionzi, Tausi Maftaha amesema huduma hiyo ni ya viwango ikilinganishwa nan chi zilizoendelea.

Daktari Bingwa huyo amesema, uanzishwaji wa huduma hiyo kwenye hospitali hiyo wanaamini itasaidia wagonjwa wanaopatiwa tiba za mionzi na dawa za dripu wanaangaliwa kwa ukaribu iwapo zinaleta madhara yoyote katika moyo.

Amesema, ujio wa huduma hiyo pia utasaidia kusaidia kupunguza gharama za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi, ambapo kwa takwimu za mwaka 2015, jumla ya wagonjwa 150 – 200 walipelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi na kwa mwaka jana, ni wagonjwa nane tu ndiyo walipelekwa nje kwa ushirikiano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Huduma hiyo inatolewa kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Ocean Road, Shirika la nguvu za Atomiki Duniani kupitia Wizara ya Afya.

Afya
Maoni