Ommy Dimpoz awashukuru shabiki zake kwa shopingi ya nguvu

|
Mwanamuziki wa bongo fleva, Ommy Dimpoz akiwa katika pozi na shabiki zake waliojishindia zawadi ya kufanyiwa manunuzi katika duka la GSM MALL
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amewafurahisha mashabiki wake wa muziki kwa kuwafanyia manunuzi maalum katika duka ya GSM yaliyopo jijini Dar es Salaam jana.
 
Mashabiki hao walijishindia zawadi hizo kutoka kwa Dimpoz kufuatia wawili hao kuwachaguliwa kupitia ukurasa wake wa Instagram wakiwa ni miongoni mwa wafuatiliaji wazuri wa muziki wake.
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz, alipiga picha na mashabiki hao kabla ya kuanza manunuzi na kuandika na kuwashukuru kwa kuwa mashabiki waaminifu.

“Na Hawa ndo Washindi maana kuna watu waliongoza kwa kujaza tag lakini hajawahi hata kutoa support japo kupost tu pale unapotoa kazi ndo maana nilisema mtag yule ambae unamuona anastahili kufanyiwa shopping ambae pia ni Fan wangu nadhani mkiingia kwenye page za hawa wawili mtaona, @imworldqueen na @kaka_wa_kingkiba mtaona ASANTENI”

Maisha
Maoni