Polisi Sudan watumia gesi za machozi kutawanya waandamanaji

|
Waandamanaji nchini Sudan wakiendelea na maandamano ya kumshinikiza Rais wao Omar Hassan Al Bashir kuondoka

Jeshi la Polisi nchini Sudan limetumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mamia ya wafuasi waliotangaza Wiki ya Maandamano ya Taifa kuongeza shinikizo la kumtaka Rais Omar Hassan Al Bashir aondokea madarakani.

Polisi wamewadhibiti wandamanaji katika Majiji makubwa mawili ambayo ni Khartoum na Omdurman ambapo baada ya Sarat Ijumaa mamia ya wananchi wameingia mitaani wakishinikiza kung'olewa madarakani kwa utawala wa Al Bashir.

Maandamano haya yalianza Disemba 19 kwa mara ya kwanza kutokana na wananchi kushinikiza kupungua kwa bei za bidhaa ikiwemo mkate pamoja na kulaani vitendo vya rushwa vinavyotajwa kushamiri nchini humo.

Takwimu zinaonesha zaidi ya watu 22 wamefariki dunia tangu kuanza kwa maandamano hayo huku jumla ya watu 800 wakiwemo wanahabari, wanaharakati, waandamanaji na Viongozi wa Upinzani wanashikiliwa.

Ghasia zimekuwa zikisababishwa zaidi kutokana na uwepo wa makundi mawili ya waandamanaji ambao ni wanaoupinga utawala wa Rais Al Bashir pamoja na wale wanaomuunga mkono.

Utawala
Maoni