Polisi yawashikilia watuhumiwa wa wizi wa hati za viwanja

|
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Muroto

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa maokosa mbalimbali ikiwemo  wizi wa hati za viwanja, kugushi na kubadili ramani za mpango mji, kubadili mpango wa matumizi ya ardhi, kuuza viwanja  na kuingilia mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu za ardhi .

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Muroto amesema katika sekta ya ardhi jijini Dodoma, kumeibuka kundi la matapeli wanaodaiwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa halmashauri wasio waaminifu kuingilia mifumo ya upimaji Ardhi, kughushi nyaraka na kuuza viwanja kwa ajili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kamishna Muroto amesema, watu hao wamekamatwa na nyaraka mbalimbali na sasa wako mikononi mwa polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi na yatakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu makosa yanayowakabili.

Uhalifu
Maoni