Rais Magufuli akutana na Mkurugenzi mstaafu wa Usalama wa Taifa

|
Rais John Magufuli alipokutana na Mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang'onda, Ikulu jijini Dar

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang'onda.

Mara baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Mwang'onda alimshukuru Rais Magufuli kwa kukubali ombi la kuzungumza naye masuala mbalimbali na kumpongeza kwa hatua kubwa aliyopiga ya kuanzisha miradi mikubwa hususan mradi wa Umeme wa Stigler Gorge ambao amesema, utakapokamilika utachangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa Uchumi.

Amesema, hakuna maendeleo bila nishati ya umeme na kwamba kwa kuwa serikali inataka kuinua sekta ya viwanda nishati hiyo itakuwa hatua muafaka katika kufikia uchumi wa kati na kuwaleta maendeleo wananchi nan chi kwa ujumla.

Utawala
Maoni