Rais Magufuli amzawadia Peter Tino shilingi mil. 5

|
Peter Tino akikabidhiwa fedha zake.

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino amekabidhiwa shilingi milioni 5 alizopewa na Rais Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa timu hiyo ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia Fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Peter ndiye aliyefunga goli lililoiwezesha Tanzania kuingia kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza na tangu mwaka huo haikufanikiwa tena mpaka mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 imepita.

Rais Magufuli ametoa fedha hizo leo alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu AFCON 2019 katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo Peter Tino aliwawakilisha wachezaji wa zamani wa timu iliyofuzu fainali hizo mwaka 1980.

Soka Tanzania
Maoni