Rais Magufuli atoa ndege ya kusafirisha mwili wa Ruge Mutahaba

|
Rais John Magufuli atoa ndege kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba

Rais John Magufuli ametoa ndege ya Serikali kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utakaopelekwa Bukoba kwa ajili ya kuzika.

Msemaji wa Falimia ya Mutahaba, Raymond Kashasha amesema hayo leo Ijumaa, Februari Mosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Ruge anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Kiziru wilayani Bukoba mkoani Kagera na atasafirishwa kutokea Dar es Salaam siku ya Jumapili, Februari 3.

Pia ametoa Ndege ya Air Tanzania kwa ajili ya watu wanaotaka kwenda kumzika Ruge ambayo itaondoka Dar es Salaam Siku ya Jumatatu, Februari 4 asubuhi kwa grarama ya Sh 600,000 kwenda na kurudi.

Usafiri
Maoni