Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa

|
Maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa huko Dodoma

Rais John Magufuli kesho Machi, 14 anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.

Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi hizo zitafanyika kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini, Masanja Kadogosa amesema maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi katika sherehe hizo yamekamilika na amewataka wananchi kujitokeza katika sherehe na waliombali na Dodoma kufuatilia matangazo yatakayorushwa mbashara kupitia vituo vya redio na televisheni.

Sehemu hii ni ya pili ya ujenzi wa reli ya katika kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya awamu tano zilizopangwa kukamilisha ujenzi wa reli hiyo itakayoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza.

Miundombinu
Maoni