Rais wa EU azungumzia sakata la Uingereza kujitoa

|
Rais wa Umoja wa Ulaya (EU), Donald Tusk

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk amesema wako tayari kuongeza muda zaidi kwa Uingereza kujiondoa katika umoja huo ikiwa Uingereza inaona ni muhimu kutafakari upya mkakati wa kujiondoa katika umoja huo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May yuko katika mkakati wake wa kuendelea kushawishi wabunge kwa mara ya tatu ili waunge mkono mpango wake wa kujiondoa Umoja wa Ulaya ambapo kura  hiyo inatarajiwa kupigwa tena Machi 20, baada ya kukataliwa mara mbili (2). 

Jana kura 413 za wabunge ziliunga mkono ombi la nyongeza ya muda zaidi kwa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU) badala ya tarehe 29 mwezi  Machi iliyopangwa awali.

Utawala
Maoni