RC na RPC Kaskazini Pemba wapata ajali Micheweni

|
Gari la Polisi mkoani Kaskazini Pemba lililogongana na Coaster lililokuwa likienda harusini

Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Kaskazini Pemba wamepata ajali baada ya gari lao kugongana na gari aina ya Coaster iliyokuwa ikienda kwenye harusi.

Ajali hiyo inadaiwa kutokea katika eneo la Sizini, wilayani Micheweni mkoani humo.

Kwa mujibu wa ukurasa wa twitter wa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar, Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, ajali hiyo imepelekea viongozi hao kupata majeraha huku wengi wao wakiwa ni abiria waliokuwa katika basi hiyo aina ya Coaster.

Ajali
Maoni