Ronaldo 'arejeshwa' Old Traford Ligi ya Mabingwa Ulaya

|
Kombe la ligi ya mabingwa ulaya (UEFA)

Hapo jana droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa mwaka 2018/19 ilifanyika huko Monaco nchini Ufaransa ambapo kubwa zaidi ni Cristiano Ronaldo akiwa na klabu yake mpya ya Juventus, wamepagwa kundi moja (Kundi H) na Manchester United ambayo ni klabu aliyowahi kuichezea katika kipindi cha nyuma ikwa chini ya Sir Alex Ferguson.

Mabingwa watetezi Real Madrid wamepangwa katika kundi G, huku timu ya AS Roma kutoka Italia ndio wanaonekana kama wapinzani wakubwa katika kundi hilo.

Jumla ya timu 32 zimepangwa katika makundi manane (A-H), na makundi yenyewe yanaonekana kama ifuatavyo;

 

KUNDI A

Atletico Madrid

Bor. Dortmund

AS Monaco

Club Brugge

 

KUNDI B

Barcelona

Tottenham

PSV

Inter Milan

 

KUNDI C

PSG

Napoli

Liverpool

Crvena Zvezda

 

KUNDI D

Lokomotiv Moscow

FC Porto

Schalke 04

Galatasaray

 

KUNDI E

Bayern Munich

Benfica

Ajax

AEK

 

KUNDI F

Man City

Shakhtar Donetsk

Lyon

Hoffenheim

 

KUNDI G

Real Madrid

AS Roma

CSKA Moscow

Viktoria Plzen

 

KUNDI H

Juventus

Man Utd

Valencia

Young Boys

 

Mechi za mzunguko wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa Septemba 18 na 19.

UEFA
Maoni