Sakata la mbegu, Naibu waziri aipa siku tatu Bodi ya Pamba

|
Zao la biashara la pamba

Bodi ya Pamba nchini imepewa siku tatu kuhakikisha kiasi cha mbegu zinazohitajika kutosheleza mahitaji ya wakulima mkoani Simiyu zinafika kwa wakati ili kuwawezesha wakulima kufanya maandalizi ya kilimo kwa wakati unaotakiwa kitaalam kwa kupanda mbegu hizo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa wakati akijibu kero za wakulima walizozianisha juu ya zao la pamba ambapo wamesema mbegu walizogawiwa na bodi ya pamba bado hazijakidhi mahitaji yao.

Kwa upande wake Maneja wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa amewatoa hofu wakulima kuhusu upatikanaji wa mbegu hizo huku mkaguzi wa viwatilifu akithibisha kuleta viwatilifu vilivyothibitishwa kuua wadudu waharibifu wa zao la pamba.

Akiongelea suala la upatikanaji wa bei nzuri ya mazao, Naibu waziri huyo amewataka wakulima wa zao hilo kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kukusanya mazao yao pamoja kwani ni moja kati ya njia nzuri ya kuwawezesha wao kupata bei nzuri.

Kilimo
Maoni