Samaki tani 11 kutoka China wateketezwa

|
Samaki ambao wameteketezwa baada ya kubainika kuwa na kemikali za zebaki

Serikali imeteketeza tani 11 za samaki zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 zilizotoka China baada ya kubainika kuwa na kemikali aina ya zebaki zenye madhara kwa jamii ikiwemo ugonjwa wa saratani na kuharibu kizazi kwa mlaji.

Samaki hao wameteketezwa baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushinda kesi iliyofunguliwa na wenye mzigo kitu kilichomfanya Waziri kuzitaka mamlaka za usimamizi ikiwemo TFDA na TBS kushirikiana ili jambo kama hilo lisijitokeze tena.

Akizungumza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, Nchama Marwa, Mkurugenzi Msaidizi wa Ulinzi Rasilimali za Uvuvi amesema kemikali zilizobainika kwenye samaki hao pamoja na madhara yake kwa watumiaji ni hatarishi kwa jamii.

Nao wamiliki wa shehena hiyo ya samaki walioshuhudia zoezi la uteketezaji wameshukuru kwa hatua hiyo na kuziomba taasisi za Serikali kushirikiana ili kuwapunguzia hasara waliyoipata.

Hadi sasa Serikali imeshateketeza tani 31 kutokana na sababu mbalimbali huku ikiahidi kuendelea na ukaguzi ili kuhakikisha samaki wote wanaoingia nchini wanakuwa salama na kuwaomba wananchi wanaopata taarifa kama hizo kuzifikisha mahali husika.

Chakula
Maoni