Samia Suluhu awataka wamiliki wa migodi kuchenjua madini nchini

|
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia madini ya Kinywe

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo, Alhamisi wakati wa kuzindua Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite) Mererani wilayani Simanjiro.

Makamu wa Rais yupo wilayani humo kwaajili ya ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.

“Pamoja na kuwekeza kwaajili ya kupata fedha na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.

Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3,730 za Kinywe.

Kwa upande mwingine Waziri wa Madini, Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.

Madini
Maoni