Serengeti Boys yachapwa 5-0 na Uturuki

|
Serengeti Boys ilikuwa ikiitumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi ya Fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwezi Aprili mwaka huu nchini Tanzania.

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo imekumbana na kipigo cha aibu cha mabao 5-0 kutoka kwa wenyeji Uturuki katika mashindano maalum ya vijana (Uefa Assist) yaliyohitimishwa leo nchini Uturuki.

Magoli ya Uturuki yamefungwa na Nuri Emre Aksit dakika ya 43, Muhammet Akpinar dakika ya 45 , Ali Akman dakika ya 52, Salih Kavrazil dakika ya 84 na Ali Karakaya akifunga bao la tano dakika ya 89.

Mashindano haya yamehitimishwa rasmi leo na sasa Serengeti Boys wanarejea nchini kujiweka tayari kwa fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Soka
Maoni