Serengeti Boys yafanya kweli Uturuki, yaichapa Australia UEFA Assist

|
Serengeti Boys vs Australia.

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano maalum ya vijana yaliyoandaliwa na Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA) yanayofahamika kwa jina la UEFA Assist.

Katika michuano hiyo inayofanyika nchini Uturuki, Serengeti Boys imeitandika Australia mabao 3-2 baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza ilipofungwa na Guinea bao 1-0.

Katika mchezo wa leo mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Edmund John, Edson Jeremiah  Kelvin John huku mabao ya Australia yakifungwa na Ryan Tegue na Noah Botic.

Azam TV kupitia channel ya Azam Sports 2 inakuletea LIVE mechi zote zinazoihusu timu hii ya Tanzania.

Soka
Maoni