Seriikali na wadau warejesha uoto wa asili Usambara

|
Utunzaji wa mazingira wilayani Muheza

Uoto wa asili katika vyanzo vya maji vilivyopo kwenye milima ya Usambara Mashariki Tarafa ya Amani wilayani Muheza,umeanza kurejea katika hali yake ya asili kufuatia juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau  kufanikisha  kuwaondoa wachimbaji wadogo wa dhahabu waliokuwa wamevamia.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa ametembelea katika vyanzo hivyo vya milima ya Usambara vilivyopo wilayani Muheza ambapo alielezwa kuwa kipindi cha nyuma hali ilikuwa mbaya kutokana na uchimbaji  wa madini uliokuwa ukiendelea.

Akitolea maelezo zaidi kuhusiana na uharibifu huo wa mazingira, Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu amesema kuwa ni vyema wananchi hao wa vijiji vinavyozunguka chanzo cha maji wakawekewa mabomba na kuingiziwa maji kwenye maeneo yao ili kuepuka uchafuzi unaoendelea kwenye vyanzo hivyo vya maji.

Akizungumza  mara baada kukagua chanzo hicho Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa  ameutaka uongozi wa Wilaya ya Muheza kwa kushirikiana na Tanga Uwasa pamoja na Wakala wa Misitu (TFS) kuhakikisha wanazidi kutunza chanzo hicho huku akiahidi kupeleka maji kwenye vijiji vinavyozunguka chanzo hicho.

Mazingira
Maoni