Serikali: Bado kuna ardhi ya kutosha kwa kilimo cha miwa

|
Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mghumba akikagua sukari katika Kiwanda cha sukari cha TPC

Serikali imesema bado kuna ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 200,000 zinazofaa kwa ajili ya kilimo cha miwa na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kuwekeza katika kilimo hicho ili kukabiliana na changamoto za upungufu wa sukari nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mghumba ameyasema hayo baada ya kutembelea Kiwanda cha Sukari cha TPC cha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema serikali iko tayari kufanya mazungumzo na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuingilia kati uzalishaji huo wa miwa.

Kwa upande wake, Afisa mtendaji Mkuu wa Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC, Jaffari Ally amesema kwa sasa wana akiba ya tani zipatazo 28,000 za sukari na uzalishaji unaendelea huku akiipongeza Serikali kwa kudhibiti uingizaji holela wa sukari kutoka nje na kuvilinda viwanda vya ndani.

Biashara
Maoni