Serikali kulipa malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi Kiwira

|
Eneo la uchimbaji makaa ya mawe Kiwira

Serikali imeahidi kuwalipa malimbikizo yote ya madeni waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.5.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Madini, Angela Kairuki baada ya kutembelea migodi hiyo na kuelezea jinsi serikali ilivyojipanga kuifufua na kufuatilia uzalishaji wake baada ya kusimama kwa muda mrefu.

Migodi hiyo ipo katika Wilaya za Kyela mkoani Mbeya na Ileje mkoani ambayo sasa itaanza upya uzalishaji wake kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Tayari Serikali imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 40 kwaajili ya kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira huku STAMICO ikiahidi kuendelea kufanya ukarabati wa mitambo mbalimbali iliyochakaa kadri ya uzalishaji kwa kutumia wafanyakazi 36 waliopo.

Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo ya kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wa migodi hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa viongozi wanaosimamia migodi hiyo akiwemo Manfred Nyamalasa ambaye ni mkandarasi wa CMG Construction wanaochimba makaa ya mawe kwenye mgodi wa Kabulo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Kanali Sylvester Poliko.  

Fedha
Maoni