Serikali ya DR Congo yatetea ulipaji wa marupurupu ya mawaziri

|
Waziri mkuu, Bruno Tshibala anayemaliza muda wake ndiye aliyesaini maagizo hayo

Serikali ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo (DRC) imetetea maagizo yanayoruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote huku idadi kubwa ya raia wake nchini humo wakiishi katika umaskini.

Katika taarifa iliyotolewa mapema jana, Serikali imesema malipo hayo ya dola 2000 kwa kiwango cha chini si ya kuwatajirisha maafisa hao kama inavyoelezwa na wakosoaji.

Taarifa hiyo imesema Serikali inayoondoka nchini DRC ilikuwa inawapatia mawaziri "kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama chakula, makazi na huduma ya afya".

Utawala
Maoni