Serikali yakiri kutumia bilioni 400 kuagiza mafuta ya kupikia

|
Serikali yakiri kutumia bilioni 400 kuagiza mafuta ya kupikia

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amekiri kwamba serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 400 kwa mwaka kuagiza mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula licha ya kuwa na mazao mengi ya mbegu za mafuta.

"Tanzania ni nchi pekee ambayo ilitoa mbegu za michikichi nchini Malaysia lakini cha kushangaza ni kwamba wale waliochukua mbegu kutoka kwetu ndiyo  wasambazaji wakubwa kuliko Tanzania," alisema Raziri Hasunga.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi utafiti wa kilimo nchini (TARI) Dkt. Jofrey Mkamilo amesema kwa sasa  wameanza mikakati ya kukuza kilimo cha mbegu za mafuta hususani zao la michikichi ili kuweza kuleta mapinduzi ya viwanda.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha TARI Naliendele Dkt. Omary Mponda akisema kuwa wakulima wakiwa tayari kupokea teknolojia wanaweza fikia azma ya Tanzania ya viwanda na kukomesha kuagiza mafuta nje ya nchi.

Kilimo
Maoni