Shirika la Posta: Tuko tayari kubadilishaji fedha za kigeni

|
Shirika la Posta likiendelea na shughuli zake za kubadilisha fedha za kigeni kupitia huduma yao ya western union

Shirika la Posta nchini limesema lipo tayari kuendesha shughuli ya kubadilisha  fedha za kigeni ikiwa ni siku chache baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kufuta leseni kwa baadhi ya maduka yanayofanya biashara hiyo kutokana na mengi kushindwa kukidhi matakwa ya sheria.

Posta Masta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta, Hassan Mwang'ombe amesema wamekuwa wakifanya biashara hiyo ya kubadili fedha za kigeni kwa muda mrefu licha ya kwamba hawatambuliki huku akisema watakuwa wanatumia kiwango cha Serikali ili kudhibiti michezo michafu.

BoT ilifungia baadhi ya maduka na kisha kutangaza huduma za kubadilishia fedha zitaendelea kupatikana kwenye benki, taasisi za fedha, Shirika la Posta na baadhi ya maduka yatakayokidhi kiwango.

Fedha
Maoni