SIDO yawanoa wakazi wa Lindi namna ya kubangua korosho

|
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylbester Mpanduji akikagua shughuli za ubanguaji wa korosho

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoani Lindi limeanza kutoa mafunzo ya ubanguaji wa korosho ghafi kwa wajasiriamali mkoani humo ili kuisaidia Serikali kuwapata wataalamu wa kutosha watakaojipatia ajira kupitia kampuni zilizopo na zitakazoingia mikataba ya ubanguaji korosho zilizonunuliwa na Serikali.

Uamuzi wa SIDO mkoani Lindi wa kutoa mafunzo bora ya ubanguaji wa korosho yamekuwa yakiunga mkono juhudi za Serikali ya kutaka korosho zote sasa zibanguliwe nchini ambapo kwa sasa wajasiriamali kutoka wilayani Lindi na Nachingwea wamepatia mafunzo hayo.

Wakieleza mafanikio ya mafunzo hayo wajasiriamali hao wameiomba Serikali kuzitatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wamewataka wajasiriamali hao kutumia fursa hiyo itakayowasaidia kujipatia ajira.

Mafunzo hayo sasa yanatarajiwa kutolewa kwa wajasiriamali waliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Lindi.

Biashara
Maoni